Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye(Mb) amesema msimamo wa Serikali ni kuifanya njia yeyote itakayotumika kwenye mawasiliano iwe salama bila ya kuingilia uhuru wa mtu/watu.
Waziri Nape ameyasema hayo wakati akizungumza na Vyombo vya Habari mara baada ya Hafla ya Ufunguzi wa Kongamano la 7 la TEHAMA Nchini lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
“Tusiwafanye watu wakashindwa kuwasiliana, lakini pia tusiruhusu uhalifu kwahiyo kama kuna hatua zozote zinachukuliwa na sekta ili kuwalinda wananchi basi Serikali inaziunga mkono hatua hizo.” Amesema Waziri Nape
“Ukiona mtu anapiga kelele ujue hajatapeliwa, mimi nakutana na watu wametapelewa milioni 10, milioni 20 na mwengine juzi ametapeliwa milioni 54, huyu ukimwambia unachukua hatua atapiga makofi lakini anaetaka kutumia mtandao huo kwa nia ovu lazima atapiga kelele.” Amesema Waziri Nape