Kwa mara ya kwanza, mwaka 2024, Mji wa Bagamoyo utakuwa mwenyeji wa Kilele cha msimu
wa Nne (4) wa Tamasha la HipHop Asili, utakaofanyika tarehe 28 – 29 Juni, 2024, katika Chuo
cha Sanaa cha Bagamoyo (TASUBA). Ambapo wataalamu wa sanaa, wasanii kutoka pembe zote za dunia watakutana kusherehekea utamaduni wa HipHop.
Mwaka huu tamasha la Hip Hop Asili limeendelea kuwa kubwa zaidi na bora, kwa kuleta
Pamoja muunganiko wa talanta za kitaifa na kimataifa katika utamadanuni wa Hiphop.
Ikijumuisha wanamuziki, wasanii wa kughani mashairi (Emcee), waandishi wa Sanaa za
machata (Graffiti), Sanaa ya umanju (Deejay), wavunjaji (Breakers), Sanaa ya upigaji wa
midundo kwa midomo (Beatboxing) na Skateboarding.
Asili Band
Mwaka huu, tamasha la Hiphop Asili kwa fahari kubwa linashirikiana na Chuo cha Muziki cha
Dhow Country Academy (DCMA) ambapo wanamuziki na wasanii wa kughani mashairi
wameshirikiana kuunda mchanganyiko wa pekee wa HipHop na muziki wa jadi/asili wa chi za
majahazi (dhow music), ili kuwapa wapenzi wa tamasha ladha ya muziki wa kipekee isiyoweza
kusahaulika.
Sanaa ya upigaji midundo kwa mdomo (Beatbox)
Utaalamu wa Sanaa ya beatboxing kwa ushirikiano kati ya wasanii kutoka jumuiya ya
beatboxing Tanzania na Msanii kutoka Uganda, kwa lengo la kujifunza zaidi sanaa hii na
kutengeneza onyesho la kipekee la Beatbox. Lakini pia kuendelea kuimarisha uhusiano wa
kitamaduni Afrika Mashariki katika kuendeleza sanaa ya Beatboxing.
Mashindano ya Breaking
Kwa kuzingatia kutambuliwa kwa Breaking kama mchezo wa Olimpiki, tamasha la Hip Hop Asili
kwa kushirikiana na StreetOff, limekuwa mwenyeji wa Mashindano ya mchezo huu Afrika
Mashariki, ambapo litajumuisha washiriki kutoka Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, na
Tanzania watakaoshindana. Washindi katika mtanange huu watapata tiketi ya kwenda
kushirkiki katika Red Bull BC One Last Chance Cypher – Rio de Janeiro (Brazil), mapema
Disemba mwaka huu.
Maonyesho ya Sanaa ya Machata (Graffiti)
Kuta za TASUBA zitabadilishwa na kupendezeshwa kwa usanifu wa grafiti kutoka kwa Wachata
kutoka Tanzania na Kactus kutoka Ufaransa. Wabobevu hawa wanatazamia kuonyesha
mtazamo Chanya kuhusu kupitia graffiti Pamoja na kupamba mandhari ya msimu wa nne (4)
wa Tamasha la Hip Hop Asili kwa masimulizi ya hadithi ya sanaa za uoni kupitia graffiti.
Burudani za Muziki
Msimu wa Nne (4) wa Tamasha la HipHop Asili, umedhamiria kuleta burudani ya muziki wa
Rap kutoka kwa kikosi bora cha wasanii ikiwa ni pamoja na:-
i. Maalim Nash
ii. Country Wizzy
iii. Machalii Watundu
iv. Sinaubi Zawose (akiwashirikisha; Stan Rhymes, Rasta Michael, na Slim the Kid) kwa
Pamoja wakiwasilisha mtindo wa kipekee wa Gogo Hip.
v. Casey kutoka Ufaransa – akishirikiana na Harley Tz, Prisca Hilonga, Slim C, na
LowKey Picasso.
Mchanganyiko na Ushirikiano wa Utamaduni: Tamasha linajitolea kukuza mabadilishano ya
kitamaduni na ushirikiano, ikionyesha urithi wa kipekee wa sanaa wa eneo hilo. Toleo la
mwaka huu litasisitiza mchanganyiko wa hip hop na muziki wa jadi wa Afrika Mashariki,
kuunda jukwaa lenye nguvu la wasanii kubuni na kusisimua.
Wito
WePresent Tanzania inawakaribisha wadau wote wa sanaa, Tarehe 28 & 29 TASUBA –
BAGAMOYO, katika siku mbili za kusherehekea utamaduni wa HipHop Tanzania. ikujumuisha
muziki, Pamoja na sanaa mbalimbali katika utamaduni huu mkongwe wa kuwaleta watu
Pamoja na kuunganisha jamii kote ulimwenguni.
KARIBU UJUMUIKE NASI.
HAKUNA KIINGILIO.