Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wamesisitizwa kuwa na nidhamu shuleni, kuzingatia masomo ili waweze kufanya vizuri kitaluma,kufaulu na kutimiza ndoto zao.
Msisitizo huo umetolewa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Mungu Tanzania REV-Dismus Mofulu alipokuwa akizungumza katika Maafali Ya Kidato Cha Sita Katika Shule ya Sekondari ALDERZGETI iliyopo Babati Mkoani Manyara
Amesema katika kipindi hiki Mmomonyoko wa Maadili Unaotokana na utandawazi,Wazazi na walezi Wanapaswa Kuwa Makini katika kuwalea watoto wao na kutowaruhusu Watoto kumiliki simu zitakazowafanya Kutokuwa Makini Katika Masomo Yao na kudunisha ustawi wao kitaluma
Aidha Amekemea vikali Mahusiano Ya Mapenzi Kwa Wanafunzi hao na kusema Kuwa Hiki ni Chanzo Kimojawapo Kinachoathiri Ustawi Wao Kitaaluma “Ninyi wanafunzi Msidanganyike Haya Maisha Ya Duniani Sio ya Kudanganyika Ni maisha Yanayopita tu mbona utayakuta huko Mbele Soma Ukimaliza Utakuta Maisha Mazuri Kule mbele yanakungoja na hao vijana ambao wanakusumbua wapo Na watazaliwa wengine wapya” Amesema Rev; Mofulu
Kwa Upande Mwingine Mkuu wa Shule Hiyo IBRAHIM AMMI Akisoma Risala katika Mafali Hayo amesema ndani ya miaka miwili Iliyopita(2022 na 2023) shule hiyo Imefaulisha wanafunzi wa kdato cha sita kwa Asilimia 100 Katika Mtihani wa Taifa”Matokeo Kidato Cha Sita 2022 Division “1 ” Zilikuwa 21,Division ” 2″ 30 Division “3” 16,Hukuna Divison “4” Wala Divison “0′ Jumla ya waliofanya mtihani walikuwa 67 Ufaulu Ulikuwa 100% ”
Matokeo Kidato Cha Sita 2023
Division “1 ” Zilikuwa 29,Division ” 2″ 70 Division “3” 8,Hukuna Divison “4” Wala Divison “0, Jumla ya Waliofanya Mtihani walikuwa 107”
“Hapa Unaweza kuona Kuna Maendeleo Mazuri Matokeo Yamekuwa Mazuri Kila Mwaka Kwa Miaka miwili Iliyopita” Amebainisha Mkuu wa Shule ya Alderzgeti Ibrahim Ammi
Katika Hatua Nyingine Wanafunzi Wanaotarajiwa kufanya Mtihani Wa Taifa Mwanzoni mwa Mwezi Mei Wamesema wamejipanga Vizuri Kuelekea katika Mtihani huo na Kuahidi kuwafanya vizuri “Nimejiandaa vizuri kwa sababu Haya yanakwenda kuwa maamuzi katika maisha yangu kwa hivo Niko Ngangari” Alisema Miriam Patric Mwanafunzi wa kidato Cha Sita Shule ya Sekondari Alderzget