Naibu katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt .Franklin Rwezimula amewataka wasaidi wa kisheria wawe mabalozi wa kuimarisha haki na wasiwe vyanzo vya kusababisha migogoro bali wawe ni watatuzi wa migogoro kwa jamii .
Dkt Rwezimula Ametoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku 15 kwa wasaidizi wa msaada wa kisheria ambapo amesema jumla ya washiriki 42 watapewa mafunzo hayo kutoka mikoa ya Dodoma ,Tanga na Singida .
Amesema jukumu kubwa la wasaidizi wa kisheria ni kujenga uwezo kwa jamii katika kutambua na kusimamoa haki na wajibu wao kwa kufanya hivyo kutakuwa na jamii yenye upendo,amani na utulivu kwani kila mmoja atalinda na kuhifadhi haki za wengine na hivyo kupunguza utendaji wa makosa .
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa LSF Amani Manyelezi amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajemgea uwezo watoa msaada wa kisheria ili kiwasaidia kuwa na uwezo wa kitoa Msaada wa Kisheria kwenye ngazi walizopo.
“Kazi yao kubuwa ni kuhakikisha kwamba wanashughulika na mashauri mengi kabla hajaenda mahakamani na tinajua wanafamya kazi kubwa kutatua migogoro ya watu na kuwasaidia wananchi kujua haki zao za msingi”
Monica Jacob na juma waziri Washiriki wa mafunzo hayo wamesema wanatanarajia kuwa mabalozi waziri wa masuala ya uelewa wa kisheria na watajikita katika kutatua migogoro inayotokea katika maeneo yao.