Mahakama nchini Misri imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela mwimbaji Shaimaa Ahmed ambae kimuziki anafahamika kama Shyma baada ya kuonekana kwenye video akiwa na vazi la ndani huku akila ndizi.
Alikamatwa mwezi uliopita baada ya video hiyo kuzua ghadhabu kwenye taifa hilo. Siku ya Jumanne alipatikana na hatia ya kuunga mkono mapenzi na kwa kuchapisha video inayokiuka maadili.
Director wa video hiyo pia nae alihukumiwa kifungo cha miaka miwili licha ya yeye kutowepo mahakamani.
Shyma alikuwa ameomba msamaha kabla kukutwa na hatia.
“Sikufikiria haya yote yatafanyika na kwamba ningeshambuliwaa kwa njia hii kali kutoka kwa kila mtu.” – Shaimaa Ahmed
Mwaka uliopita mahakama nchini Misri ilawahukumu wacheza dansi watatu wanawake miezi sita gerezani baada ya kuwatuhumu kwa kuchochea ngono kwenye video ya muziki.
Mwimbaji mwingine anakabaliwa na kesi kwa kueneza uvumi kuwa maji ya mto Nile yanaweza kumfanya awe mgonjwa.
JPM AONYA WASICHANA WANAOJIACHIA KWENYE VIDEO,SIX-PACK ZA WANAUME JE?, BONYEZA PLAYA HAPA CHINI KUMTAZAMA.