Msomi wa Masters Zawadi Zakaria Masanja mkazi wa Dar es salaam ameamua kuja na mbadala wa kutumia wembe wakati wa kufanya usafi wa mwili badala yake utatumia lotion kupaka sehemu unayotaka kutoa nywele au vinyweleo kisha kunawa na maji.
Zawadi alipata ujuzi huo kupitia mtandao baada ya kutafuta kazi za ma ofisini kwa muda mrefu bila kufanikiwa.
Zawadi anaeleza..”Imekuwa ni ndoto yangu ya muda tangu nikiwa masomoni China kufikiria ni kipi nitakileta kwa Jamii yangu kinipe kipato bila ya kuajiriwa, baada ya kutuma maombi ya Ajira bila mafanikio nikaanza kujifunza mbinu za Usafi wa mwili mtandaoni, niligundua madhira wanayapitia wanawake na Wanaume wakati wa kujisafisha”
“Bidhaa hii inatumiwa na watu wote bila kujali jinsia zao ndio maana hata mtu niliyeamua kufanya nae kazi ni Mwanamke kutoka Uswahilini Zai wa kijiwe nongwa, furaha yangu ni kuona baada ya kukosa kazi za maofisini leo nimeleta ajira sio tu kwangu na hata kwa wengine”– anaeleza Zawadi