Leo July 10, 2018 Moja ya taarifa ubwa kutoka nchini Burundi ni kuwa Wasichana 16 kutoka mikoa ya nchi hiyo waliokuwa wanashiriki katika fainali ya mashindano ya kumpata msichana mrembo Burundi (Miss Burundi) wamejiondoa katika shindalo hilo.
Wamedai kuwa kuna utata mkubwa katika maandalizi ya mwaka huu huku wakitolea mfano ahadi za vitu atakavyopewa mrembo wa kwanza na wa pili.
Washindi waliahidiwa gari jipya, kiwanja chenye ukubwa wa mita mraba mia nne na pesa taslim lakini hayo yote hayajaandaliwa na Waandaaji wa mashindano ambao ni shirika la Burundi Event.
Fainali hiyo ilipagwa kufanyika July 21, 2018 imesogezwa mbele hadi July 28 lakini pia kuna uwezekano wa kutofanyika kwa shindano hilo kwa mwaka huu.
Tume anayoitaka Mke wa Bilionea Erasto Msuya iundwe