Radio show ya asubuhi ya Power Breakfast @CloudsFMTZ leo July 19 2023 imefanya mahojiano na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Arusha na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo nafasi yake kwenye matumizi ya mtandao wa Internet wakati akiwa Rais.
Mstaafu Kikwete alisema kwenye utawala wake mwaka 2005 hadi 2015 vita dhidi ya rushwa alipambana nayo sio tu kwa Watuhumiwa kupelekwa Mahakamani lakini pia aliwekeza kwenye mkongo wa Taifa uliosambaza mtandao wa internet kwa kiwango kikubwa ili kuuondoa utaratibu wa kulazimisha Wananchi kufata huduma za kiserikali dirishani na badala yake kutumia mtandao ili kupunguza mianya ya rushwa kati ya Mtoa huduma na mpewa huduma.
Alipoulizwa kuhusu misemo yake maarufu ikiwemo ‘akili za kuambiwa changanya na zako’, Mstaafu Kikwete alijibu kama ifuatavyo “Ujumbe wangu pale ni kwamba unapopewa nafasi ya uongozi usiwe unafanya yale unayoambiwa tu, utasikia mengi lakini baada ya pale tafakari uweze kuchambua chuya na mchele, kwenye nafasi ya uongozi tatizo lake ni kwamba kama sio muangalifu utaumiza Watu”
Kipindi hiki maarufu cha asubuhi ambacho husikika kuanzia saa kumi na moja alfajiri hadi saa nne asubuhi kimefanya mahojiano haya Jijini Arusha ambako kunaendelea Mkutano unaojadili demokrasia Barani Afrika uliohudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu Kikwete.
Fanya kupita kwenye Youtube ya CLOUDS MEDIA ili utazame Interview hii kubwa ya siku iliyofanywa na Wakali wa hizi kazi.
View this post on Instagram