Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya mrisho Kikwete Ameiomba wizara ya Utamaduni Sanaa na michezo kwa kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu nchini kutathimini idadi ya uwepo wa wachezaji wengi wa kigeni kwenye timu moja kama inathari yoyote kwani kwa upande wake ameona idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni umeathiri kwa kiasi chake kungaa kwa nyota wa kitanzania.
Dkt Kikwete amesema amewahi kuiomba Shirikisho wakati akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe za siku ya wananchi shirikisho lijaribu kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni lakini cha kushangaza badala ya kupungua idadi ikaongezeka kutoka nane mpaka hivi sasa ipo kumi na mbili.
“Ukifuatilia ligi yetu ya nyumnbani utasikia majina yanayotajwa ni ya wachezaji wa kigeni tu kwa yanga utawasikia wakina mayele sijui Diara wakina Juma Shabani ukienda, Simba utasikia Mara Baleke Mara Chama lakini huwezi kusikis wachezaji wa kitanzania Naamini Naibu waziri wa michezo kijana wangu Hamis Mwinjuma umisikia na mtalifanyia kazi”