Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu zake za rambirambi kwa Mke wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Mama Dorcas Membe akielezea alivyopokea taarifa za kifo cha Membe kwa mshtuko na huzuni kubwa.
Dr. Kikwete amesema “Nimemfahamu Membe miaka mingi, tumetoka nae mbali na tumesaidiana kwa mengi, Familia zetu, na mapito ya maisha yetu yamehusiana sana, Bernard KamilliusMembe alikuwa ni Mtu wa msaada mkubwa kwangu katika maisha yangu ya kikazi na kisiasa”.