Hayo yamesemwa na Maria Pinto, Katibu wa Wizara ya Bahari na Uvuvi Msumbuji akisema kuwa ambaye ameliambua kongamabo katika mji mkuu, Maputo kwamba, nchi hiyo hupoteza kati ya dola milioni 60 hadi 70 kila mwaka kutokana uporaji huo.
Amesema nchi yake inapaswa kutafakari kwa kina kuhusu njia ya kukabiliana na tatizo la uvuvi haramu.
Pinto alisisitiza jukumu kubwa la uvuvi katika maisha ya watu, haswa kupitia uvuvi wa ufundi, na mchango wake katika uchumi wa taifa.
Katibu Mkuu alibainisha kuwa uvuvi una mchango mkubwa wa kijamii na kiuchumi kwa maisha ya watu na katika kuzalisha fedha za kigeni, hasa uvuvi wa kienyeji, kwani kwa ujumla unachangia karibu asilimia 40 ya samaki wanaovuliwa na kuajiri zaidi ya asilimia 90 ya wavuvi.
Mwezi jana jarida la North African Post lilimnukulu Samuel A. Jinapor Waziri wa Ardhi na Maliasili Ghana akisema kuwa Kanda la Ghuba ya Guinea ya Afrika Magharibi hupoteza dola bilioni 26 kutokana na uvuvi haramu na biashara haramu ya rasilimali za baharini.
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO linakadiria kuwa uvuvi haramu, usioripotiwa na usiodhibitiwa husababisha upotezaji wa tani milioni 11 hadi 26 za samaki kila mwaka.
Hasara za kiuchumi ni kati ya dola bilioni 10 hadi 23.Samaki inachukuliwa kuwa bidhaa muhimu kwa kuhakikisha uhakika wa chakula. Meli za kigeni ndizo kutoka Ulaya na bara Asia zinasemekana kuhusika pakubwa katuka uvuvi haramu barani Afrika.