Viongozi wawili waandamizi wa wanajihadi wameuawa katika operesheni ya pamoja na vikosi vya kikanda katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado nchini Msumbiji, jeshi linasema.
Mmoja wao alikuwa Abu Kital ambaye “alishikilia wadhifa wa naibu kamanda wa operesheni za kundi la Ahlu-Sunnah wal Jama`a (ASWJ)” mwingine alikuwa Ali Mahando, ambaye pia alishika wadhifa wa juu katika kundi hilo., taarifa ya jeshi ilisema.
Aliongeza kuwa magaidi walivamia kitengo cha magari cha FADM ambacho kilikuwa sehemu ya safu ya kijeshi inayoelekea katika wadhifa wa utawala wa Cabo Delgado wa Quiterajo mnamo saa 08.30 siku ya Jumanne.
Gari la kuongoza lilipinduka, na wanajihadi walilichoma moto hata hivyo, waliokuwa ndani ya gari hilo hawakujeruhiwa.
“hivi sasa hatua zinaendelea kukusanya habari kuhusu mienendo mingine ya magaidi ambayo itatolewa kwa vyombo vya habari kwa wakati unaofaa”.
Jeshi la Msumbiji na vikosi vya washirika, ikiwa ni pamoja na wanajeshi wa Rwanda na ujumbe wa kijeshi kutoka kambi ya kikanda ya kusini mwa Afrika ya Sadc, wamekuwa wakiendesha operesheni katika jimbo hilo lililoathiriwa na wanajihadi.
Msumbiji imekuwa ikipambana na waasi wenye uhusiano na kundi la Islamic State tangu Oktoba 2017.
Zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kuyahama makazi yao huku wengine zaidi ya 4,000 wakiuawa katika kipindi hicho.