Simon Happygod Msuva sio jina geni masikioni mwa wapenda soka wa Tanzania hususani wapenzi na mashabiki wa klabu ya Dar Es Salaam Young African. Simon Msuva ni mkali wa soka ambaye anaitumikia Yanga na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, lakini huenda unamfahamu uwanjani pekee lakini haya huyafahamu.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Simon Happygod Msuva ndiye staa ambaye anashikilia rekodi ya mchezaji bora wa Ligi Kuu msimu uliyopita pamoja na rekodi ya kuwa mfungaji bora wa msimu uliyopita. December 1 katika exclusive interview na millardayo.com Simon Msuva anatupa mambo matatu ambayo huyafahamu kuhusu yeye.
1- Baba na mama yake mwanzoni walikuwa hawamsapoti kucheza soka walitaka ajikite katika masomo zaidi “Nilianza kucheza soka toka nasoma shule ya msingi wazazi walikuwa hawataki nicheze soka walitaka nisome tu ila baada ya kumaliza form 4 waliamua kuniunga mkono” >>> Msuva
2- Fedha yake ya kwanza kubwa kushika ni laki tatu ambayo alisajiliwa na klabu ya Moro United wakati huo na kuamua kuitoa sadaka ” Nilisajiliwa na Moro United kwa laki tatu lakini baada ya kushauriana na baba na mama tukaamua kuitoa sadaka yote ili mungu anifungulie milango” >>> Msuva
3- Kutokana na umahiri wake uwanjani aliwahi kupewa zawadi ya gari na mashabiki wa Yanga ” Sikutarajia kuwa mashabiki watanipa zawadi ya gari ila nilihisi kwani washawahi kuniuliza napenda gari gani kati ya Nissan X-Trail, Passo, Opah na Altezza nikachagua Altezza, siku wakanipigia simu kwenda nikakabidhiwa funguo za gari” >>> Msuva
Hii ni sauti ya Simon Msuva
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.