Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya stori ni hii kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Padri apiga marufuku maharusi kupaka shedo’
#MTANZANIA Kanisa katoliki Parokia ya Hananasif K'ndoni yapiga marufuku maharusi kupaka 'lipstick' wakati wa misa pic.twitter.com/G2oV6j4bpm
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
Gazeti la Mtanzania limeripoti kuwa waumini wanawake wanaokwenda kufunga ndoa katika kanisa Katoliki Parokia ya Hananasif Kinondoni, jijini Dar es salaam wamepigwa marufuku kupaka rangi ya mdomo “lipstick” wakati wa ibada ya misa takatifu ya ndoa.
Gazeti hilo limeongeza kuwa uamuzi huo ulitangazwa juzi jioni na Paroko wa Parokia ya Hananasif Kinondoni jijini Dar es salaam Padri Gasper Mtengeti, wakati wa ibada ya misa ya kumwombea marehemu Rose Michael iliyofanyika kanisani hapo.
Aidha gazeti hilo limeongeza kuwa kutokana na hali hiyo Padri Mtengeti aliwataka wanawake waache kupaka rangi wakati wa misa takatifu ambapo alitoa sababu tatu zinazotokana na Liturijia ya Ekaristi Takatifu (utaratibuwa uendeshaji wa ibada) chini ya kanisa Katoliki.
Padri Mtengeti alieleza sababu hizo kuwakataza maharusi wa kike kujipaka rangi ya mdomo kuwa rangi hiyo inayopakwa huwa inasalia katika chombo kinachobeba divai ambayo kiimani kwa dhehebu hilo ni damu ya yesu kristu.
Sababu nyingine iliyoelezwa kupitia gazeti hilo ni pamoja na kuwa rangi ya mdomo huwa inachanganyika na damu ya Yesu wakati wanapokunywa kitendo ambacho si chema mbele za Mungu, sababu nyingine ni kuwa rangi hizo hubaki kwenye kitambaa cheupe kinachotumika kufuta kikombe cha hostia baada ya kuguswa na midomo.
Unaweza kuzipitia habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya leo hapa chini
#MWANANCHI Ripoti ya Lugumi ilikuwa iwasilishwe kwenye mkutano wa bunge unaoendelea, sasa itawasilishwa mkutano ujao pic.twitter.com/2BGEnYCnFC
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#MWANANCHI Baada ya Uingereza kujitoa EU, balozi wa nchi hiyo awatoa hofu Watanzania asema haitapunguza uwekezaji pic.twitter.com/ZQcvlmtabB
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#MWANANCHI Mkurugenzi mkuu TAKUKURU, Mlowola asema waliochota Escrow hawako salama kwa kuwa anaendelea kuchunguza pic.twitter.com/Ei45mnEA5Q
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#MWANANCHI Tundu Lissu amepandishwa ktk mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka ya uchochezi pic.twitter.com/BPHui8uKEZ
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#MWANANCHI Watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu ya helium nchini Tanzania pic.twitter.com/mq6P6PSgdU
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#NIPASHE Kwa May 2016 ajali za bodaboda ni 879, 224 zilisababisha vifo 76 ambao ni wastani wa watu watatu kila siku pic.twitter.com/kdjS3nA4uX
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#MWANANCHI Kamati kuu CCM imeagiza kamati ya wabunge wa chama kuwapa barua za kujieleza wasioudhuria vikao vya bunge pic.twitter.com/a3067vgHdY
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#MWANANCHI Serikali yakomalia mikutano ya siasa kuzuiwa kufanyika hadi jeshi la polisi litakapoona inafaa kufanyika pic.twitter.com/5CSpeXgfSm
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#MTANZANIA Serikali inatarajia kufuta posho zote zinazolipwa kwa kamati zinazohusika na michakato ya zabuni pic.twitter.com/Pla3V4gNVp
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#RaiaMWEMA Hatimaye Koplo Deogratias Mbango ambaye Rais aliagiza apandishwe cheo, sasa amepandishwa na kuwa Sajenti pic.twitter.com/TLNY8Yiqpq
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#JamboLEO Hoja ya kutaka CUF ifutwe yakosa jibu bungeni, naibu waziri mambo ya ndani asema hilo linamhusu msajili pic.twitter.com/NQubxT13NS
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#TanzaniaDAIMA JPM atengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Singida, Fikiri Avias ndani ya saa 24 baada ya kumteua pic.twitter.com/u1VfnxwwRX
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#NIPASHE Muswada mabadiliko sheria ya ununuzi ambao unaziba mianya ya ulaji wa fedha za umma umewasilishwa bungeni pic.twitter.com/oVTYteOc0V
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#NIPASHE Athari za kujitoa kwa Uingereza EU zimeanza kujitokeza nchini baada ya wateja wa pauni kukauka ghafla pic.twitter.com/F6P4fz9gQ9
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
#NIPASHE Watendaji 12 Z'bar akiwemo Naibu mhasibu mkuu wa serikali wasimamishwa kutokana na upotevu mkubwa wa fedha pic.twitter.com/VcXHQT5oGp
— millardayo (@millardayo) June 29, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JUNE 29 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUITAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE