Sergei Karaganov, mtaalamu mwenye ushawishi mkubwa wa Sera za kigeni nchini Urusi, anamtaka Rais Vladimir Putin kuwa na msimamo mkali zaidi kuhusu matumizi ya Silaha za Nyuklia dhidi ya nchi zinazounga mkono NATO katika vita vya Ukraine.
Aidha Karaganov amesema Urusi inapaswa kuonyesha wazi nia yake ya kutumia Silaha hizo dhidi ya Mataifa ya Magharibi ili kuzuia kuendelea kwa vita.
Katika mahojiano na gazeti la Kommersant la Urusi, Karaganov amependekeza kwamba shambulio dogo la Nyuklia dhidi ya Nchi mwanachama wa NATO linaweza kufanyika bila kusababisha vita vya Nyuklia vya jumla.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa mchakato huo ni wa lazima ili kulinda maslahi ya Urusi, akionya kuwa vita vya Ukraine vinaweza kuipeleka Nchi hiyo kwenye hatari kubwa endapo haitarejesha uwezo wa kuzuia mashambulizi makubwa.