Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Saada Mkuya amesema Serikali ya Zanzibar imeazimia kuhakikisha Kila Mgeni anaeingia Zanzibar kuhakikisha anakata Bima ya Lazima ya Zanzibar Travel Insurance inayosimamiwa na Serikali ya Mapinduzi kupitia ZIC ambayo itamlazimu Mgeni kuikata akiwa nchini mwake wakati akijianda kufika Zanzibar.
Mkuya amesema sio Jambo geni na Zanzibar pekee ambayo Mgeni ,Mtalii hutakiwa kukata bima za lazima ambazo husaidia pindi wanapopata majanga ya kiafya na kusema mataifa mbali mbali wamekua wakiifaya hivyo ili kumhakikishia Mgeni, Mtalii Nchini na kwamba jambo hilo linatekelezwa kwa matakwa ya kisheria na inataarajiwa kuanza Mwezi Septemba tarehe Mosi.
kwa Upande wake Meneja wa ZIC Hamida Salum amesema Bima hiyo itakatwaa kwa Dola $44 na pindi Mgeni ,Mtalii hatohitaji kutibiwa Tanzania serikali itasimamia Gharama za kumtibu popote anapohitaji.