Mtandao wa masoko 42 Markets upande wa fedha na mitaji umepata msaada wa dola milioni 10 kama mtaji wa kupanua huduma zake kutoka Convegence Partners, ambayo ni moja ya taasisi kubwa za mitaji duniani ambazo zinawekeza kwenye sector ya teknolojia barani Afrika. Hii ni baada ya kufunga mfuko wake uliyokuwa unalenga kukuza tecnolojia (CPDIF) uliyokuwa na kiasi cha dola za marekani million 296.
Afisa Mtendaji wa 42 Markets Group Andries Brink amesema “Hii ni imani kubwa katika nia njema ya kuwekeza kwenye miundombuni ya teknolojia ya fedha lakini pia kukuza masoko madogo,”.
Moja kati ya soko kubwa la taasisi hiyo ni kampuni ya masoko ya huduma za mitaji na ushauri Andile (UK, andile.net), ambayo huleta pamoja wataalam wa masoko na mitaji kusaidia idara za biashara na hazina ndani ya benki ili ziweze kutumia vizuri idara zao za Technolojia ya Habari (IT).Kwa sasa kapuni hiyo inahudmia benki Kuu na Benki za uwekezaji ndani ya Africa, Wingereza, Ulaya, Australia na India.
Kampuni zingine ni pamoja na early-stage platform bussiness FXFlow (SA, fxflow.co) ambayo ni jukwaa linahusika na kuongeza thamani kwa waagizaji wa mizigo nje kwenye masoko yaliyodhibitiwa kisheria na Mesh (Uholanzi, Mesh.trade) ambayo inahusika na kutenganisha masoko asili ya fedha na masoko ya kisasa ya fedha na mitaji.
Brandon Doyle, Afisa Mtendaji Mkuu wa Convengece Partners alionegeza kuwa “Huu ni mmoja wa uwekezaji wetu mkubwa kwenye eneo la mapinduzi ya kidigitali na masoko ya mtandao, tunaiona 42 Markets ikiibuka mshindi kwenye eneo hili. Mtandao wao wa kmpuni una historia kubwa wa ukuwaji wa herufi mbili mfululizo na uongozi makini ambao unauelewa mkubwa wa masoko ya hisa,”
DFIs ambayo ipo Ulaya, Marekani na Afrika ni wawekezaji wakubwa kwenye (CPDIF) ambapo Brink amesema (Huu ndo mtaji tuliokuwa tunausubiri. Tunawasiliana na wawekezaji hawa kuangalia maeneo na fursa zingine za kushirikiana,”
Christian Roelofse, Afisa anayehusika na Uholanzi alisema FMO imeridhika na hatua ambazo Covengence partners inafanya kutambua na kuwasaidia wajasiliamali katika bara la Afrika.
“Kupitia uwekezaji wao kwenye kampuni kama 42 markets, tunaamini kwamba uelewa wa teknolojia ya fedha utaongezeka barani Afrika. Na Tunajivunia kushirikiana na kampuni bunifu ambazo zinatafuta majibu ya mahitaji ya kisasa,”