Sudan imekubwa na kukatika kwa mtandao huku wengi wakilaumu kundi la wanamgambo wanaopambana na jeshi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi 10 nchini humo.
Kikosi cha (RSF) kimekana kuhusika.
NetBlocks, shirika linalofuatilia uhuru wa mtandao, lilisema kwenye X, kumekuwa na “kuporomoka kwa muunganisho wa intaneti” nchini Sudan.
Inakuja wakati kundi la wadukuzi ambao ni wanaharakati wa Sudan kuilenga Uganda kwa kumkaribisha kiongozi wa RSF, Mohamed Hamdan Dagalo.
NetBlocks ilisema imepata usumbufu kwa huduma za watoa huduma za intaneti Uganda Telecom na MTN, ingawa ripota wa BBC katika mji mkuu Kampala alisema hakuona matatizo yoyote.
Nchini Sudan, baadhi ya watu wameripoti kutoweza kupata mtandao tangu Ijumaa lakini hali imekuwa mbaya zaidi tangu wakati huo.
Vyombo vya habari vinayoungwa mkono na serikali vimeilaumu RSF.