Mwandishi na mtangazaji nguli wa Dira ya Dunia na Idhaa ya Kiswahili ya BBC Salim Kikeke ametangaza rasmi kuondoka katika Shirika la Utangazaji Uingereza BBC baada ya kufanya kazi kwa miaka 20.
Salim Kikeke mwenye umri wa miaka 44 ameaga rasmi wakati akifanya matangazo yake ya mwisho ya Dira ya Dunia ambapo wameagwa pamoja na wenzake Salma Kassim aliyefanya kazi BBC kwa miaka 44 pamoja na Mariam Omar ambao nao wamemaliza utumishi wao.