Mtanzania Diana Paul Chando amechaguliwa kuwa Balozi wa Umoja wa Africa (AU) kwenye Kitengo cha Amani na Ulinzi (Peace & Security).
Diana ambaye ameteuliwa leo nchini Ethiopia ndiye Mtanzania wa Kwanza kijana kupata nafasi ya Ubalozi katika AU, ambapo katika uteuzi huo pia kuna Mabalozi wa mataifa mengine pia wameteuliwa.
“Naomba support ya Serikali, Sekta binafsi, kwenye kufanya kazi kwa uthubutu kwenye kuendeleza umoja kwenye nchi za Afrika, miongoni mwa vigezo vya kuteuliwa ni kwa sababu natokea nchi ya amani, utulivu hivyo wakaona wanichague ili nihamasishe amani kwenye nchi zenye vita,”. amesema Diana (akiwa Ethiopia).
Mbali na Ubalozi huo, pia Diana ni Mwanasheria, Mwanadiplomasia, pia alishwahi kufanya kazi Umoja wa Mataifa (UN).