Application ya NALA imetajwa na Jarida la Biashara la Afrika (BUSINESS ELITES) kwenye kumi bora ya Application bora za Afrika zinazojishughulisha na maswala ya kifedha, APP ambazo teknolojia yake ni kubwa, imara na yenye ubunifu ambapo Application hiyo ilianzishwa na Benjamin Fernandes.
NALA ambayo ilianzishwa mwaka 2018 nchini Tanzania ambayo mpaka sasa imeshinda Tuzo 7 huku ikitumika kwenye mataifa mawili ya Afrika ambayo ni Tanzania na Uganda, hivi karibuni itafungua huduma yake ya kutuma na kupokea pesa kimataifa duniani.
NALA Ni APP iliyopo google play store ambayo moja ya kazi yake kubwa ni kukusaidia kupanga miamala yako yote ya fedha kutoka kwenye account zako zote ziwe za Benki au za simu za mkononi.
Mpaka sasa kwa Tanzania ina downloads zaidi ya laki moja huku nyota za ubora zikifikia alama 4.7 kati ya 5 kutoka kwenye idadi ya Watu zaidi ya elfu moja mia nane walioiongelea, size yake ni 6.0 M na ni APP ambayo hauhitaji kuwa na Internet kuitumia, internet itatumika pale tu unapoipakua kuiweka kwenye simu yako lakini baada ya hapo unadunda nayo bila kutumia internet.
MAAJABU: DUKA LISILO NA MLANGO WA MBAO WALA WA CHUMA NA HAKUNA ANAYETHUBUTU KUDOKOA HATA KIBIRITI, BONYEZA PLAY KULITAZAMA HAPA CHINI