TAKUKURU Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na ofisi ya Mwendesha Mashtaka, inatarajia kumfikisha mahakamani aliyekuwa Afisa Mtendaji wa kata ya Tyuka Jijini Dodoma kwa Tuhuma za kufanya ubadhilifu wa shilingi Million 32.9 ikiwa ni makusanyo ya ushuru wa madini ya ujenzi ambayo ni Kunyume na Sheria ya Uhujumu Uchumi.
Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma SOSTENES KIBWENGO wakati akizungumza ofisini kwake.