Baraza la Mitihani la Tanzania limefungia vituo vya mitihani viwili sawa na 0.01% vya vituo 18,645 vya mitihani vilivyothibitika kupanga na kufanya udanganyifu katika Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA) 2022 kwa mujibu wa Kifungu 4(8) cha Kanuni za Mitihani mwaka 2016 hadi hapo Baraza litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa Mitihani ya Kitaifa.
Vituo hivyo ni Busara S/M, Halmashauri ya Magu-Mwanza na Musabe S/M, Jiji Mwanza-Mwanza.