Taarifa kutoka Mtwara ambazo zimethibitishwa na jeshi la Polisi ni kuhusu Mtumbwi ambao umezama wakati ukivuka kutoka kitongoji cha Ng’wale kwenda ng’ambo ya pili ambapo ndiyo sehemu waliyokuwa wanashukia abiria waliokuwepo.
Tayari watu 21 wamefikishwa katika hospital ya mkoa wa Mtwara kwa matibabu ambao wote ni wakina mama pamoja na mtoto mmoja wa kiume wa mwaka 1 huku waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo wakiwa ni wakina mama 3.
Mtumbwi huo unahisiwa ulikuwa na abiria 24 ambapo pamoja na wahusika wawili wa mtumbwi huo kwa pamoja, jumla ya watu waliokua kwenye mtumbwi ni 26 ambapo Polisi wanasema kina mama hao walikua wanatoka kutafuta samaki kwa ajili ya biashara.
Jeshi la polisi bado linamtafuta aliekua anauendesha huo Mtumbwi ambae inasemekana aliogelea na kutoweka baada ya mtumbwi kuzama.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika ingawa baadhi ya abiria wanadai ni upepo mkali na mvua iliyokuwa inanyesha kwenye eneo hilo.
Kwa muendelezo wa taarifa hii kaa karibu na MillardAyo kwenye facebook, twitter na instagram kwa jina hilohilo la @millardayo ili uwe wa kwanza kupata hizi taarifa baada tu ya kunifikia.