Rose Sagauli (7) mwanafunzi wa awali shule ya msingi Mji Mwema iliyopo mtaa wa Mji Mwema Halmashauri ya Mji wa Njombe amechomwa moto mikono na kaka yake Zedekia Maguchi (18) mwanafunzi wa kidato cha tano kwa tuhuma za kula ndizi mbili alipokuwa na njaa.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mji Mwema Leonard Mkupi ameithibitishia Ayo TV juu ya tukio hilo ambapo amesema baada ya kumhoji mtoto alieleza kuchomwa mikono kwa sababu ya kuingia ndani na kula ndizi mbili baada ya kusikia njaa.
“Mtoto alipokuwa na njaa aliingia ndani akachukua matunda aina ya ndizi mbili na kuzila halafu kaka yake akamkamata na kumfunga mikono yote miwili ndipo alipowasha jiko la kuni na kumchona”amesema Mkupi
Katibu tawala wilaya ya Njombe Agatha Mhaiki ameonya familia zinazomaliza mikasa ya ukatili kindugu na kuitaka jamii kutoa taarifa kwenye mamlaka dhidi ya vitendo vya ukatili huku akiahidi kuchukuliwa sheria kwa yeyote atakayebainika kuhusika kwenye vitendo hivyo.
“Ukatili hauna ujamaa huo ni ukikwaji wa haki za binadamu lakini pia ni unyama kwa hiyo tukumbushane na kusema hapana juu ya vitendo hivi”amesema Mhaiki