Polisi Mkoani mara wamelazimika kuanza kufanya kazi ya ziada kwa kuwaagiza Trafiki wanapokagua Mabasi wakumbuke kuwakumbusha Abiria kutoamini Abiria waliokutana nao kwenye basi na kukubali kula vyakula wanavyopewa na Abiria hao wasiowafahamu.
Hii ni baada ya matukio matatu kutokea kwenye Mabasi yanayokwenda Mkoani Mara ambapo Watu mbalimbali wameibiwa pesa na mali mbalimbali baada ya kulishwa vyakula vya kuwalevya na kisha Wezi kuwasachi na kuwaibia kila kitu walichonacho.
Moja ya hayo matukio matatu ni tukio la Mtoto anayekadiriwa kuwa na miaka 15-18 kufanikiwa kumlewesha Mwanaume Mtu mzima na kumuibia shilingi milioni mbili na laki saba (2.7m) “Matukio haya yametokea kwenye mabasi yanayotokea Mwanza kuja Mara, Abiria wanalishwa madawa kwenye biskuti, ndizi na vingine, akifika huku anakuwa tayari ameshazirai” ——— RPC Mara, Longinus Tibishubwamu.