Joseph Bukombe Mabula ni Mtoto ambaye amelelewa na nyani kwa zaidi ya miaka miwili katika pori la msitu wa Bukombe Mkoa wa Geita, inadhaniwa ni baada ya kutupwa na Mzazi wake hadi hapo alipookotwa na Watu wa misitu na baadaye kukabidhiwa kwa Maafisa wa Ustawi wa Jamii.
Mwanzoni hakufahamika majina yake ila waliamua kumuita Mabula kwa kuwa alizaliwa msimu wa mvua kwa kabila la Wasukuma na Bukombe ndio msitu aliookotwa, kwa sasa Mabula analelewa na kituo cha Upendo Daima cha Malimbe Mwanza.