Mtoto mwenye miaka tisa aliyejulikana kwa jina la Abas Jeras ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Lemba Mkoani Kigoma amefariki dunia baada ya kulipuliwa na bomu la kurusha na mkono aliloliokota.
‘’Mtoto huyo akiwa anachunga mifugo aliokota bomu la kutupwa na mkono kwa kutotambua ni bomu wakati anarejea nyumbani alikua akilichezea ndipo bomu hilo lilipuka na kupelekea kifo chake’’ James Manyama RPC Kigoma