Saidi Mangara ni mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 15, anaeishi Tabata DSM, akiwa darasa la nne alijigundua kuwa ana kipaji cha kuchora, baadae akajikuta akahamishia michoro kwenye uhalisia zaidi na hapo akaanza kutafuta mabox na kutengeneza maumbo ya nyumba, kwa sasa Saidi ana uwezo wa kusanifu majengo ya nguvu ya aina mbalimbali na anauza kazi zake kwa bei tofauti, fedha anazopata zinasaidia kuendesha familia kwani anakiri kipato cha Baba yake sio kikubwa.
Said anatamani kuwa Engineer mkubwa hapo baadae lakini anatambua ili atimize malengo yake ni lazima azingatie elimu, hivyo anasoma kwa bidii na anapenda sana masomo ya sayansi, anasema licha ya hali ngumu ya kimaisha nyumbani kwao haijawahi kukatisha tamaa yake ya kutimiza ndoto alizonazo.