Serikali imefanikisha zoezi la kuanza kuto huduma za afya katika Kituo kipya cha afya Makowo kilichopo Halmashauri ya Mji wa Njombe kilichojengwa kwa zaidi ya shilingi milioni 600 mara baada ya kufungwa vifaa tiba ambapo Watotoo wawili wa kike wamezaliwa salama kwa njia ya upasuaji kituoni hapo na mmoja wa kwanza amepewa jina la Samia.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Yesaya Mwasubila kwa niaba ya Mkurugenzi amesema kituo hicho cha afya kimefungwa vifaa vya milioni 270 mpaka kuanza kwake kutoa huduma huku akiwashukuru Wananchi kwa kuwa wavumilivu tangu kituo kilipoanza kujengwa mwaka 2017 kutokana na nguvu zao pamoja na mapato ya ndani.
Kutokana na furaha walionayo Wananchi kwa kituo hicho kuanza kutoa huduma na kusaidia Wanawake wawili kujifungua Watoto wa kike kwa mara ya kwanza, ndipo Wananchi wakaamua Mtoto wa wa kwanza kumpa jina la Samia kama sehemu ya kumshukuru Rais Samia na wapili akipewa jina Iluminatha jina la aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashauri hiyo huku Mbunge wa jimbo hilo Deo Mwanyika akitoa wito wananchi kutunza vifaa na kituo hicho.
“Kituo hiki kitahudumia watu wengi niombe vifaa vitunze na tumepamabana Halmashauri tutapata magari mapya mawili na kwa mamlaka mliyonipa ninyi wananchi gari moja ni hapa Makowo”