Waziri wa sheria wa Uturuki ametangaza Alhamisi kwamba mtoto wa kiume wa Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, anatarajiwa kurejea Uturuki kujibu mashtaka ya ajali mbaya ya barabarani iliyosababisha kifo mjini Istanbul.
Yilmaz Tunc, waziri wa sheria wa Uturuki, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Ankara ilifanya mazungumzo na mamlaka ya mahakama ya Somalia juu ya kumrudisha Mohamed Hassan Sheikh Mohamud. “Katika siku zijazo, mshtakiwa atakuja Uturuki, na mchakato wa kesi utafanyika”, Tunc alisema.
Hapo Novemba 30, Mohamud alimgonga Yunus Emre Gocer, mwendesha pikipiki katika wilaya ya Fatih huko Istanbul, wakati mtoto huyo wa Rais akiendesha gari yenye namba za leseni ya kidiplomasia. Muathirika huyo mwenye umri wa miaka 38 alipelekwa hospitali mara moja, ambako alifariki Disemba 6.
Lakini update kutoka kwenye vyombo vya habari zinasema kuwa rais wa Somalia anasema mwanawe hakutoroka Uturuki baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabara kuu huko Istanbul.**Amemshauri mwanawe kurejea na kujiwasilisha mahakamani, ambayo imetoa kibali cha kukamatwa.
Rais Hassan Sheikh Mohamud alisema katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press kwamba mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 40, ambaye ni daktari, alisalia katika eneo la ajali na kubaki Istanbul kwa siku kadhaa baadaye.
“Ilikuwa ajali. Hakukimbia, na aliajiri wakili kwa ajili hiyo,” rais alisema.
“Na hapakuwa na hati ya kukamatwa. … Kwa hiyo, ana biashara na alitoka nje ya nchi.”
Mwathiriwa, Yunus Emre Gocer, msafirishaji pikipiki mwenye umri wa miaka 38, alifariki hospitalini Desemba 6, siku sita baada ya kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na mtoto wa rais, Mohammed Hassan Sheikh Mohamud, kwenye barabara kuu yenye shughuli nyingi mjini Istanbul. .