Mtu wangu wa nguvu kila mtu anatamani na anapenda kuishi maisha mazuri tena hasa maisha ya mjini leo April 25, 2016 kupitia Hekaheka ya Clouds FM, Geah Habib ametuletea stori ya binti wa darasa la kwanza alipelekwa Dar es salaam kwa dhumuni la kusoma lakini alipofika Dar es salaam mambo yalikuwa tofauti, stori kamili unaipata hapa millardayo.com.
Mtoto huyo wa darasa la kwanza ameeleza jinsi alivyotolewa morogoro mpaka Jijini Dar es salaam…….. >>>’Mimi naitwa Jesca na mama yangu anakaa Ngalimila, Morogoro huku Dar nilikuja na mama Lusungu alivyokuja nyumbani kunichukua aliniambia nije kukaa naye huku Dar‘:-Jesca mtoto wa miaka 9
‘Baada ya kufika huku Dar ndio Mama Lusungu aliniambia, wewe hujui kupika, kuosha vyombo, hujui kusoma wala kuandika, mimi nimeamua kuondoka nimeondoka kwa Mama Lusungu kwa sababu amesema kwamba amenifukuza‘:-Jesca mtoto wa miaka 9
‘Mimi nilikuwa nasoma darasa la kwanza Ngalimila huyu mama Lusungu ndio akanileta huku Dar, sisi kwetu tuko watoto nane wasichana tuko wanne na wakiume wako wanne‘:-Jesca mtoto wa miaka 9
STORI KAMILI BONYEZA PLAY HAPA CHINI NIMEKUWEKEA NA UNAWEZA UKATUACHIA COMMENT YAKO…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIMISS HII YA KALAPINA KUHUSIANA NA KUFAHAMU VINGI KUHUSINA NA MATIBABU YA CHID BENZ ITAZAME HAPA HII VIDEO….