Mtu mmoja ameuawa na wengine Sita wamejeruhiwa huku nyumba zaidi ya 15 zikichomwa Moto baada ya kuibuka mapigano ya Wakulima na Wafugaji Jamii ya Kisukuma katika Kijiji cha Alabama kata ya Itete wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro.
Tukio hilo limetokea Disemba 27,2021 ambapo wafugaji wanaodaiwa kuingiza Mifugo hiyo katika shamba la wakulima katika Skimu ya umwagiliaji ya Kijiji
Ayo TV na Millard Ayo .com imesafiri zaidi ya Kilomteta 400 kutoka Morogoro mjini hadi katika kijiji hicho yaliyopotokea mapigano hayo ambapo majeruhi wa tukio hilo wanaeleza ilivyokua.
Mathew Massele ni Mkuu wa wilaya ya Malinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo anathibitisha kutokea tukio hilo huku Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Antipus Mgungusi amefika kwenye kijiji hicho kwa lengo la kutoa pole kwa wafugaji na wakulima kutokana na tukio hilo.