Watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia akaunti feki ya “facebook” yenye jina la Mama Janeth Magufuli Mke wa Rais Magufuli.
Watuhumiwa Sophia Mwaluanda [22] Mfanyabiashara na Mkazi wa Sistila Jijini Mbeya na MPanji Mwinyimvua [38] Mkazi wa Manzese Jijini DSM.
Akizungumza Jijini Mbeya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amesema Watuhumiwa wamekamatwa April 28,2020 katika operesheni na msako uliofanywa huko eneo la Ikuti Sokoni, Kata ya Ikuti, Jijini Mbeya.