Gazeti la Mtanzania leo Novemba 14 limeandikwa kichwa cha habari kinachosomeka hivi; “.. Utafiti watibua wagombea urais 2015.. January aupinga, Zitto amwambia aache siasa.. Keissy ashangaa Wasira kutosomeka katika ripoti..”
Kupitia mtandao wa Twitter, hiki ndicho kilichoandikwa na mhariri Absalom Kibanda na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba;
J. Makamba : “@absakibanda Unaelezeaje suala la gazeti lako kunukuu kinyume kabisa na mtu alivyosema? Umeambiwa. @kevarist @zittokabwe @MariaSTsehai”
A. Kibanda : “@JMakamba Nimeambiwa kaka. Badala ya kuandika JM kahoji wao wakaona umepinga utafiti.”
J. Makamba : “@absakibanda Si kweli. Na nimesema specifically sipingi. Heshima ndogo niliyobakiwa nayo na Mtanzania imeisha.”
A. Kibanda : “@JMakamba You judge the paper kwa kosa ambalo msingi wake ni kauli yako?! Worldwide media zinafanya makosa hayo ya tafsiri”
J. Makamba : “@absakibanda makosa yanatokea, ni kawaida na yanasameheka. Kupindisha makusudi kwa malengo mahsusi ni dhambi kwa wasomaji, tasnia na mhusika”
A. Kibanda : “@JMakamba Kaka unless silijui hilo. Siwezi kuruhusu gazeti naloongoza likuhujumu wewe au mwingine yeyote. Hata awe Membe anayenichukia”
Unahitaji kupata kila stori inayonifikia mtu wangu? Ni rahisi sana, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook