Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu wamerudishwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu kwa ajili ya muendelezo wa kesi yao ya Ugaidi na Uhujumu Uchumi ambayo inatarajiwa kutolewa uamuzi leo.
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Jaji Joachim Tiganga baada ya mara ya mwisho kuibuka kwa mabishano ya kisheria juu ya upokelewaji wa kielelezo cha sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Baada ya mabishano hayo yalichukua takribani saa sita, Jaji Tiganga aliahirisha kesi hiyo na leo Januari 10, 2022 atatolea uamuzi wa pingamizi hilo kama Mahakama ipokee sare hizo ama lah.
Mbali na Mbowe washitakiwa wengine ni Halfan Bwire, Mohamed Ling’wenya na Adamu Kasekwa.