Kaimu Mkurugenzi wa Lishe katika Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Moshi ametoa onyo kali kwa Wanaume wanaoendeleza tabia ya kupenda kunyonya maziwa ya Wake zao wanaonyonyesha na kuwataka kuacha mara moja kwani kufanya hivyo wanawapunja watoto.
Dkt. Moshi ameyasema hayo wakati akitoa mada kwenye mkutano na Wanahabari wa SADC na kusema Wanaume wamekuwa wakibuni mbinu mpya kila siku kufanikisha adhima yao.
Amesema kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya wanaume kupendelea kunyonya maziwa ya Mama huku wengine wakiwapa masharti kwamba wanyonyeshe Mtoto ziwa moja na lingine wabakishiwe wao.
Amesema Wanaume lazima watambue kuwa maziwa ya Mama ni tiba na kinga kwa Mtoto huku akishangazwa na tabia ya Wanaume wanaopenda kuyanyonya akihoji maana yao hasa ni nini?.