Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila imefanya upasuaji wa kupandikiza magoti na nyonga bandia kwa wagonjwa 140 kuanzia Novemba 2023 hadi Aprili mwaka huu ambapo waliopandikizwa nyonga ni 40 na magoti ni 100.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Upasuaji wa hospitali hiyo Dkt. Godlove Mfuko ametoa taarifa hiyo wakati akielezea namna Idara ya Mifupa na Ajali ilivyoisaidia jamii kupata huduma za matibabu.
Amesema idara hiyo inatoa huduma mbalimbali ikiwemo kurekebisha mifupa iliyovunjika, paja na huduma zingine za kibobezi ikiwemo upasuaji wa kiuno na upasuaji wa mgongo.
Mgonjwa akifanyiwa upasuaji anaruhusiwa katika kipindi cha siku tatu hadi tano kulingana na aina ya upasuaji aliofanyiwa.