Mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani anayekipiga katika klabu ya FC Bayern Munich ya kwao Ujerumani Thomas Muller, December 18 ameingia katika headlines baada ya kuamua maamuzi tofauti ila ni pigo kwa klabu ya Man United. Muller ambaye ana mudu kucheza nafasi ya winga, mshambuliaji pamoja na kiungo ameamua kuongeza mkataba na FC Bayern, maamuzi ambayo yamezima ndoto za Man United kumpata nyota huyo.
Uongozi wa klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani kupitia tovuti yao wamethibitisha kuamua kuwaongezea mikataba wachezaji wake wanne, ambao ni Jerome Boateng, Xabi Alonso, Javi Martinez na Thomas Muller ambaye katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August 2015 alihusishwa kwa karibu kutaka kujiunga na Man United.
Uamuzi wa Muller na wachezaji wenzake wa kuongeza mkataba hadi mwaka 2021, uliambatana na kauli ya Thomas Muller ambayo huenda ikawa inalenga vilabu vyote ila inatajwa kuilenga Man United kwani ndio walikuwa wanahusishwa kwa karibu kutaka kumsajili staa huyo “Ninajivunia na nina furaha kukwambia kuwa nimeamua kuongeza mkataba na FC Bayern Munich, hadi 30/06/2021” >>>Muller
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.