Mama Mzazi wa Mwanamke aitwae Swalha ambaye inadaiwa ameuwawa kwa risasi na Mume wake Jijini Mwanza amesema Mtoto wake alikua nyumbani kwake ( kwa Mama) saa chache kabla ya kuuwawa kwa risasi na kwamba alisikia Mume wa Mtoto wake huyo akimfokea alipompigia simu.
Akiongea akiwa nyumbani kwake Kirumba Mwanza, Mama Mzazi wa Marehemu amesema Mume wa Mtoto wake alimpigia simu na kuomba aongee na Mke wake na kusema yafuatayo “Mke wangu leo nimeshinda njaa toka asubuhi niko melini nasikia sana njaa naomba uwahi uje unipikie chakula, nilisikia kama anafokafoka kidogo kwamba ana njaa sana, kuhusu ugomvi huwa ni simu… mpaka saa tisa za usiku anapiga simu, Marehemu alikuta missed calls 42 Mwanaume anapiga tu simu na alivyopokea ile simu akaanza kumtukana”
Mama huyu amesema ndoa ya Mtoto wake ilikua inatimiza miezi mitano kwani ilifungwa December 2021, Interview nzima ya Mama akisimulia yote ipo hapa