Takriban miaka 128 iliyopita, mwizi na mlevi, anayejulikana kwa jina la Stoneman Willie’ aliyefariki kwa matatizo kufeli kwa figo kwasababu ya ulevi akiwa katika jela ya Pennsylvania mnamo Novemba 19, 1895 hatimaye maiti yake yaamuliwa kuzikwa .
Kabla ya kufariki aliipa mamlaka jina la uwongo alipokamatwa, utambulisho wake halisi na unabaki kufichwa hadi sasa.
Kulingana na shirika la habari la BBC Mwili wake ulihifadhiwa kwa kuzungushwa ndani ya kipande cha nguo (mbinu ya kale iliyotumiwa kuhifadhi maiti hasa katika nchi ya Misri -ikijulikana kama Mummyification) kwa bahati mbaya na mtaalamu wa maiti anayejaribu mbinu mpya za kuhifadhi miili (zinazowafanya wafu wawe na muonekano wa mtu aliye hai kwa kuingiza kimiminika maalumu mwilini mwao (new embalming techniques), kulingana na Nyumba ya Mazishi ya Auman.
Akiwa amevalia suti nyeusi bwana huyo ameonyeshwa kwenye jeneza huku akiwa na kitambaa kingine chekundu kifuani mwake. Nywele na meno yake vimeendelea kuwa sawa, na ngozi yake imechukua muonekano wa ngozi yake.
Nyumba ya mazishi ilikuwa imeomba serikali ruhusa ya kuuhifadhi mwili huo badala ya kuuzika ili kufuatilia mchakato wa majaribio ya kumtambua.
Hadi sasa, hakuna mengi yaliyojulikana juu yake .