Jackie Chan amewatuliza mashabiki baada ya wasiwasi kuibuka kuhusu kuonekana kwake kwenye picha zilizochapishwa mapema mwaka huu.
Muigizaji na staa huyo anayefahamika kwa filamu zikiwemo Police Story, Rush Hour na Who Am I?, alipigwa picha akiwa na mvi, jambo lililowafanya mashabiki kutafakari kuhusu afya yake.
Chan sasa amezungumzia wasiwasi huo kwenye mitandao ya kijamii, akishiriki msururu wa picha zinazoakisi kazi yake katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 70 mapema wiki hii.
Alisema sura yake ya uzee mwanzoni mwa mwaka huu kwa kweli ilikuwa sehemu ya utaftaji wake wa uhusika wa filamu.
“Si muda mrefu uliopita, marafiki wengi waliona picha zangu za hivi majuzi kwenye mtandao, na wote walikuwa na wasiwasi kuhusu afya yangu,” nyota huyo aliwaambia wafuasi wake milioni 6.2 kwenye Instagram.
“Nataka kuchukua fursa hii kuwafahamisha kila mtu, usijali! Ni mwonekano tu wa wahusika wa filamu yangu ya hivi punde. Mhusika ananihitaji kuwa na nywele nyeupe, ndevu nyeupe na kuonekana mzee.
“Kwa miaka mingi, nimekuwa tayari kujaribu vitu vipya kwa ajili ya filamu, haijalishi ikiwa ni shida au mwonekano wa mafanikio kwa mhusika.”