Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa wito mwishoni mwa wiki wa kupiga marufuku safari za nje ya nchi kwa Wabunge na watumishi wa umma ili kuokoa fedha kwa mambo mengine yenye kipaumbele zaidi.
Ameyasema hayo alipokuwa akituma vifaa katika Taasisi ya Petroli ya Uganda-Kigumba (UPIK) ambapo nchi hiyo inatarajia kutoa mafunzo kwa wataalam wa ndani katika utafiti wa mafuta.
Uganda inatarajia kuanza kusukuma mamilioni ya mapipa ya mafuta mwaka ifikapo mwaka 2025 kutoka kwenye hifadhi yake kubwa ya mafuta, lakini rais hakufurahishwa na kwamba taasisi ya mafunzo bado haijakamilika kutokana na ukosefu wa fedha.
“Waambie watumishi wa umma na wabunge waache kusafiri nje ya nchi. Pesa zinapotea katika safari za nje na bado Kigumba inalilia pesa,” alisema, kwa mujibu wa taarifa ya vyombo vya ndani.
Rais Museveni pia alipendekeza kusimamishwa kwa posho zote, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Daily Monitor.