Kylian Mbappe amethibitisha kuwa hataongeza mkataba wake PSG. Mshambulizi huyo anataka kuondoka katika klabu hiyo msimu ujao wa joto wakati mkataba wake utakapokamilika na aliambia Gazzetta dello Sport kwamba klabu hiyo inafahamu uamuzi wake.
Alisema:
“Sikuomba kuuzwa au kwenda Real Madrid.
Nilithibitisha tu kwamba sitaki kuamsha mwaka wa ziada uliotarajiwa kwenye mkataba. Hatujawahi kuzungumza juu ya kuongezwa tena na PSG, lakini nina furaha kubaki hapa msimu ujao.”
Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi hakufurahishwa na mshambuliaji huyo kuweka hadharani uamuzi wake na inasemekana alitaka kumuuza kwa Real Madrid mapema mwaka huu. Aliiambia Le Parisien:
“Tunamtaka abaki, lakini hawezi kuondoka bure. Hayo ndiyo yalikuwa makubaliano yetu ya mdomo, na aliyaeleza hadharani kwenye mahojiano. Kwa hiyo haina mjadala. Nilishangaa sana kujua kwamba alikusudia kuondoka bure. ”
Al Hilal inasemekana walituma ofa ya Euro milioni 300 kwa Kylian Mbappe na PSG ikakubali ofa hiyo. Walakini, mshambuliaji huyo alikataa kuhama na hakuruhusiwa kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza wakati wa maandalizi ya msimu mpya.