Nahodha wa Liverpool Virgil van Dijk amezungumzia hali yake ya kandarasi ya muda mrefu, akidokeza kuwa hana aina yoyote ya taarifa mpya kwa sasa.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi anasalia kuwa mchezaji muhimu sana kwa Liverpool, na bila shaka mashabiki watakuwa na hamu ya kumuona akiweka mustakabali wake katika klabu hiyo.
Wachezaji wa Liverpool walilazimika kutengaishwa mara kadahaa baada ya mchezo wa Man United!
Bado, Van Dijk ameulizwa kuhusu mkataba wake wa Liverpool, ambao unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu, mara kadhaa msimu huu, na jibu lake limekuwa lile lile kila mara.
Van Dijk alisema: “Hakuna kitu (kwenye mkataba). Lakini nina utulivu juu yake, kama nilivyosema miezi kadhaa iliyopita.
Tutaona kitakachotokea katika siku zijazo na kwa wakati huu sijapata update yoyote.”
LFC hakika inahitaji kumbakisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye anasalia kuwa mmoja wa mabeki bora zaidi duniani, lakini hii ni sakata nyingine kubwa ambayo inaonekana kuendelea kuvuta.