Mbunge wa Geita kupitia CCM, Joseph Kasheku ameshauri mabilioni yanayowekezwa na Serikali kwenye miradi ambayo haizalishi kuwekezwa kwa watu wa hali ya chini.
“Tumeona Serikali kipindi kilichopita imekuwa na miradi mikubwa ya mabilioni ya pesa ambayo haina impact yoyote kwenye Taifa na Watanzania wale wa chini hatuoni faida ya miradi mikubwa ambayo Serikali imewekeza mabilioni” Musukuma
“Ni kwasababu pengine Wasomi mnashindwa kutafakari kwamba mnapojenga masoko, mastendi makubwa ya mabilioni, ile ni huduma, sasa nyie mnaviweka kama vitega uchumi” Musukuma