Mswada wa kufadhili bajeti ya serikali kuu unaoungwa mkono na rais mteule Donald Trump, umeshindwa kupitishwa na baraza la wawakilishi.
Darzeni ya warepublican walikataa kufuata maagizo ya rais mteule Donald Trump, kutaka mswada huo upitishwe jana alhamisi.
Hatua hiyo imepelekea baraza la wawakilishi kukosa mwelekeo namna ya kuzuia serikali kuu kufungwa, hatua inayoweza kuvuruga mipangilio ya sherehe za krisimasi kwa wamarekani.
Kukosa kupitishwa mswada wa bajeti, ni hatua inayoweka taaswira namna chama cha Republican kinaweza kuwa na wakati mgumu katika uatawala wake kuanzia mwaka ujao, Trump atakapoingia madarakani.
Chama cha Republican kinadhibithi baraza la wawakilishi na senate