Polisi Arusha wamesema kwenye uchunguzi wa awali kuhusu kifo cha David Mtaita (30) ambaye alikua akifanya kazi kama Muuguzi kwenye Hospitali ya Wilaya ya Meru Arusha, umebaini kwamba alikua na msongo wa mawazo uliotokana na madeni aliyokua nayo.
Kamanda wa Polisi Arusha Justine Masejo amesema ——— > “kabla ya Mtaita kujinyonga alijidunga kwanza dawa ya kupunguza/kuondoa maumivu na kisha ndio akajining’iniza kwenye ceiling board kwa kutumia kamba pazi”
“Naomba msijichukulie maamuzi ya kujinyonga badala yake mnaweza kwenda maeneo maalum kupata ushauri nasaha” ——— Kamanda Masejo.