Wakati Serikali ikiwa imeweka sawa sakata la viwanda vya saruji bungeni, baadhi ya wadau wametoa maoni yao na kusema kuwa muunganiko wa viwanda vya saruji sio njia ya kutawala soko.
Maoni hayo yanafuatiwa na ile kauli ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dk Ashantu Kijaji ambapo alisema, wizara hiyo ilifuata sheria na kanuni zote baada ya kupokea ombi la muunganiko.
Katika maoni hayo ambayo pia vimetajwa vifungu vya sheria, wadau wa masuala ya Maendeleo wamesema “Kwa mujibu kifungu cha 11 kifungu kidogo cha 2 cha sheria ya Tume ya Ushindani (FCC) ya mwaka 2018 pamoja na kifungu cha 1 kifungu kidogo cha 2 kinatoa vigezo kwa kampuni zinazoungana na zimekidhi vigezo vyote vilivyowekwa hapo juu ili kuwasilisha ombi lao bila kujali ombi lao la awali kukataliwa au kukubaliwa. Hii inamaanisha kuwa kampuni mpya haiwezi kuwa na zaidi ya asilimia 35 ya soko,”.
Hata hivyo pia wamebainisha uwezo na hali ya uzalishaji wa viwanda vya saruji nchin–-“Maweni Limestone (Huaxin) 2,200,000 (20%), Dangote Cement 2,200,000 (20%), Tanzania Portland Cement (Twiga) 2,100,000 (19%), Tanga Cement (Simba) 1,200,000 (11%) Mbeya (Bamburi) 700,000 (6%) DSM Cement (Camel) 700,000 (6%) Lake Cement (Nyati) 660,000 (6%) Kisarawe Cement 300,000 (3%),”
“Kwahiyo nilichokiona katika kuthibitisha kile alichoongea Mheshimiwa Waziri. Muunganiko hautaweza kutawala soko. Kuongeza asilimia 19 kwenye asilimia 11 kutafikia asilimia 30 tu. Hii imekuwa wazi kwangu sasa. Pia niliona mara nyingi sana Tanga na Twiga wakisaidia jamii mbalimbali nchini, huku viwanda vingine vikiwa havifanyi hivyo,”.