Waandamanaji kutoka chama cha Democratic Labour Confederation (CDT) walikusanyika katika uwanja wa kihistoria wa Casablanca wakielezea kutoridhishwa na kupanda kwa bei pamoja na kupunguzwa uwezo wa ununuzi
Mamia ya watu waliandamana Jumapili katika mji mkuu wa kiuchumi wa Morocco, Casablanca kupinga kupanda kwa gharama za maisha katika taifa hilo la Afrika Kaskazini na kutaka hatua zichukuliwe na serikali, waandishi wa habari wa shirika la AFP wamesema.
Vyama vya wafanyakazi vinashutumu makubaliano ya kijamii yaliyohitimishwa mwaka jana lakini hayakutumika.
Hapo awali, CDT ilitaka kufanya maandamano ya kitaifa huko Casablanca lakini maandamano hayo yalipigwa marufuku na mamlaka za mitaa, amesema Tarik Alaoui El Housseini, mjumbe wa Baraza la Kitaifa la CDT “Tumeamua kususia kazi,” ameleza.
Waandamanaji wengine pia walisafiri kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hadi Casablanca kwa ajili ya maandamano hayo.
Waandishi wa AFP walishuhudia makabiliano kati ya maafisa wa usalama na waandamanaji lakini walisema maandamano hayo yalimalizika bila ya kutokea tukio kubwa.